Awe ana shahada ya kwanza ya tiba ya mifugo (BVM) kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Baraza
Awe amefanya mafunzo ya uanagenzi
Ada ya usajili ya TZS. 50,000/=
Mtanzania aliyesoma nje ya nchi anaweza kusajiliwa baada ya kuwasilisha vyeti vya taaluma na kutakiwa kufanya mafunzo ya uanagenzi na hatimaye kufanya na kufaulu mtihani wa Baraza
Daktari asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa kwa muda na kufanya kazi kama za utafiti, mtaalam muelekezi, mkufunzi, na wenye ujuzi maalum kwa muda maalum
Daktari asiye Mtanzania anaweza kupewa usajili wa kudumu na kufanya kazi za uwekezaji katika tiba ya afya ya wanyama kwa masharti ya kufanya kazi...
Awe na shahada ya tiba ya mifugo.
Awasilishe usajili wake toka mamlaka inayosimamia taaluma ya veterinari kutoka nchi anapotoka.
Awe na kibali cha kufanya kazi hapa nchini kutoka mamlaka husika.
Awe amefanya na kufaulu mtihani wa ufaulu wa Baraza.
Atatakiwa kulipa ada ya usajili ya US$ 5...
Awe ana stashahada ya afya ya wanyama; au Stashahada ya afya ya wanyama na Uzalishaji katika Tropiki (Diploma in Tropical Animal Health and Production) ama Stashahada ya Afya ya wanyama na Uzalishaji
Awe amefanya na kufaulu mtihani wa Baraza
Ada ya kuorodheshwa ni TZS. 40,000/=.
Awe amesomea astashahada ya afya ya wanyama au astashahada ya afya ya wanyama na uzalishaji katika chuo kinachotambuliwa na Baraza.
Ada ya kuandikishwa ni TZ sh 40,000/=.
i) Daktari asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanya kazi kama za utafiti, kama mtaalam muelekezi, mkufunzi, na wenye ujuzi maalum kwa muda maalum (Temporary registration).
ii) Daktari asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanya kazi za uwekezaji katika tiba ya afya ya wanyama kwa masharti...