Majukumu ya Baraza yameaanishwa katika kifungu cha 5 cha Sheria ya Veterinari Na. 16, ya Mwaka 2003 ambayo ni pamoja na;
a. Kusajili, kuorodhesha na kuandikisha wataalam, wataalam wasaidizi na kusajili vituo vya huduma ya afya ya wanyama;
b. Kumshauri na kutoa mapendekezo kwa Mhe. Waziri kuhusu jambo lolote linarohusu utaoji huduma za afya ya wanyama;
c. Kusimamia maadili na mienendo ya wataalam;
d. Kuweka sifa za mafunzo ya taaluma ya veterinari, vyuo na taasisi zinazotoa mafunzo ya wataalam wa afya ya wanyama;
e. Kusimamia huduma ya tiba ya wanyama;
f. Kushirikiana na taasisi zingine kutambua mitaala katika taaluma ya veterinari; Kuweka viwango vya huduma ya tiba ya wanyama, mipaka ya kutoa huduma kwa ngazi mbalimbali za wataalam wa afya ya mifugo na viwango kwa masomo yanayohusu taaaluma;
g. Kuhamasisha maendeleo ya taaluma ya tiba ya wanyama;
h. Kutunza na kutoa taarifa zinazohusu taaluma ya tiba ya wanyama;
i. Kuandaa mitihani ya taaluma kwa ajili ya usajili, kuandikishwa na kuorodheshwa;
j. Kufuatilia utendaji kazi wa madaktari, wataalam wasaidizi na wasaidizi wa wataalam wa mifugo;na
k. Kutekeleza jambo lolote jingine kwa mujibu wa Sheria.