Mtihani wa ufaulu kwa madaktari wa mifugo waliosoma nje ya Nchi

Kwa mujibu wa Kifungu cha 20(1) & (2) cha Sheria ya Veterinari SURA 319 na Kanuni ya 7(2) ya kanuni za (Taratibu za Usajili wa Madaktari wa Mifugo na Madaktari Wabobezi), 2005 na kanuni za (Taratibu za Usajili wa Madaktari wa Mifugo na Madaktari Wabobezi)(Marekebisho), 2011 Madaktari wa mifugo waliohitimu nje ya Nchi wanatakiwa kufanya  mtihani wa ufaulu. Ikiwa mtahiniwa atafeli mtihani, Baraza hutoa fursa ya mwisho kwa mwombaji kufanya mtihani tena.