Baraza la Veterinari husajili, kuandikisha na kuorodhesha wataalam wa kada mbalimbali za taaluma ya mifugo kulingana na vigezo vifuatavyo:-
USAJILI WA MADAKTARI WA MIFUGO
- Awe na Shahada ya udaktari wa Wanyama kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Baraza.
- Awe amemaliza mafunzo ya uanagenzi katika vituo vinavyotambuliwa na Baraza.
- Mhitimu aliyesoma nje ya nchi, awe amefaulu mtihani wa Baraza.
KUORODHESHA WATAALAMU WASAIDIZI
- Awe na Stashada ya Tiba na Uzalishaji wa Mifugo kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Baraza.
- Awe amemaliza mafunzo ya uanagenzi katika vituo vinavyotambuliwa na Baraza.
- Mhitimu aliyesoma nje ya nchi, awe amefaulu mtihani wa Baraza.
KUANDIKISHA WASAIDIZI WA WATAALAMU WASAIDIZI
- Awe na Astashahada ya Tiba na Uzalishaji wa Mifugo kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Baraza.
- Mhitimu aliyesoma nje ya nchi, awe amefaulu mtihani wa Baraza.
Kwa kujisajili bofya hapa >https://mimis.mifugo.go.tz/frontend/web/user/sign-in/login