Baraza la Veterinari husajili vituo mbalimbali vya huduma za mifugo kulingana na vigezo vifuatavyo: -
USAJILI WA VITUO VYA HUDUMA ZA MIFUGO
- Awe na daktari msimamizi anayetambulika na Baraza
- Awe na Mtaalam Msaidizi au Msaidizi wa Mtaalam Msaidizi anayetambulika na Baraza.
- Mkataba wa kisheria kati ya mmiliki na wataalam wanaotoa huduma katika kituo husika.
- Awe na orodha ya ukaguzi (Inspection Checklist) iliyosainiwa na daktari wa Halmashauri ya Wilaya husika baada ya kukaguliwa.
- Uwepo wa vifaa tiba kulingana na aina ya kituo kama atakavyoelekezwa na Daktari wa Mifugo wa Halmashauri ya Wilaya.
Kwa kujisajili bofya hapa >> https://mimis.mifugo.go.tz/frontend/web/user/sign-in/login