Baraza la Veterinari Tanzania lilianzishwa kwa mujibu wa kifungu cha 3 cha Sheria ya Veterinari Na. 16, ya Mwaka 2003 baada ya kufuta Sheria ya Madaktari Wapasuaji wa Wanyama (CAP 376) ya Mwaka 1958, na majukumu yake ni kusimamia taaluma ya vaterinari na huduma za afya ya wanyama ili kuhakikisha kuwa wafugaji wanafaidika na mifugo yao.

Msajili wa kwanza wa Baraza la Veterinari ni Dkt. Ponela Mlelwa aliyehudumu kwa kipindi cha miaka kumi (10) kutoka mwaka 2004 hadi Februari 2014; akifuatiwa na Dkt. Bedan Masuruli aliyehudumu kwa miaka minane (8) kutoka Februari 2014 hadi Aprili 2022, na kwa sasa anaehudumu Ofisi hiyo ni Dkt. Amani J. Kilemile alianza mwezi Septemba, 2022.