Kuhuisha Usajili kwa Madaktari wa Mifugo na Madaktari Wabobezi wa Mifugo

Kwa mujibu wa Kifungu cha 23(1) cha Sheria ya Veterinari SURA 319, kila Daktari wa Mifugo au Daktari Mbobezi wa Mifugo aliyesajiliwa atahuisha usajili wake kwa kulipa ada ya kila mwaka.

Ada ya kuhuisha inapaswa kulipwa katika mwaka wa kalenda.

Pale ambapo Daktari wa Mifugo au Daktari Mbobezi wa Mifugo aliyesajiliwa atashindwa kulipa ada ya kuhuisha kila mwaka kabla ya kuisha kwa cheti kilichopo cha usajili, Baraza linaweza kuhuisha usajili iwapo maombi yatafanywa ndani ya miezi sita baada ya kumalizika kwa muda;

Baada ya kipindi hicho cha miezi sita, Daktari wa Mifugo au Daktari Mbobezi wa Mifugo aliyesajiliwa atakuwa hajahuisha usajili wake, Baraza litasimamisha usajili wake kwa mwaka mmoja, na iwapo baada ya mwaka mmoja Daktari wa Mifugo au Daktari Mbobezi wa Mifugo atashindwa kuhuisha usajili, basi Baraza, kwa kuzingatia Kifungu cha 27 cha Sheria ya Veterinari, litafuta usajili na kuondoa jina lake kwenye daftari la usajili.

Kiasi cha ada za kuhuisha kitalipwa kwa mujibu wa Kanuni za Veterinari (Ada na Tozo Nyingine) ya Mwaka, 2015.

Kuomba kuhuisha bofya hapa>>>>>http://mimis.mifugo.go.tz

 

Kuhuisha kwa Wataalamu wa Wasaidizi na Wasaidizi wa Wataalam Wasaidizi wa Mifugo

Kwa mujibu wa Kifungu cha 37(1) cha Sheria ya Veterinari SURA 319, kila Mtaalamu Msaidizi aliyeorodheshwa au aliyeandikshwa atahuisha kwa kulipa ada ya uhuishaji kila mwaka.

Ada ya kuhuisha inapaswa kulipwa katika kalenda ya mwaka; pale ambapo mtu aliyeorodheshwa au aliyeandikishwa atashindwa kulipa kabla ya mwisho wa muda uliopo wa uorodheshaji au uandikishaji, Baraza linaweza kufanya uorodheshaji au uandikishaji huo ikiwa ombi litafanywa ndani ya miezi sita baada ya kumalizika kwa muda.

Iwapo baada ya miezi sita, mtu aliyeandikishwa au kuorodheshwa hajafanya kuhuisha uorodheshwaji au uandikishaji wake, Baraza litasimamisha uorodheshwaji au uandikishwaji kwa muda wa mwaka mmoja na ikiwa baada ya kipindi hicho cha mwaka mmoja Mtaalamu Msaidizi au Msaididi wa Mtaalam Msaidizi atashindwa kuhuisha basi, Baraza, kwa kuzingatia Kifungu cha 34 cha Sheria ya Veterinari, litafuta uorodheshaji au uandikishaji na kuamuru kuondolewa kwa jina la mtu husika katika Orodha au Lisiti ya uandikishaji.

Kiasi cha ada za kuhuisha kitalipwa kwa mujibu wa Kanuni ya Veterinari (Ada na Tozo Nyingine) ya Mwaka, 2015.

Kuomba kuhuisha bofya hapa>>>>>http://mimis.mifugo.go.tz

 

Kuhuisha kwa Wahimilishaji

Kwa mujibu wa Kanuni ya 5(1) ya Kanuni za Veterinari (Utoaji Leseni kwa Wahimilishaji) ya Mwaka 2011; kutakuwa na ada ya kuhuisha leseni itakayolipwa kila mwaka na Mhimilishaji aliyeidhinishwa.

Daktari wa mifugo aliyesajiliwa, mtaalamu msaidizi aliyeorodheshwa na msaidizi wa mtaalam msaidizi aliyeandikishwa hawatalipa ada ya uhifadhi kulingana na kanuni ya 5(2) ya Kanuni za Veterinari (Utoaji Leseni kwa Wahimilishaji) ya Mwaka 2011

Kuomba kuhuisha bofya hapa>>>>>http://mimis.mifugo.go.tz

 

Kuhuisha kwa Wakaguzi wa Nyama

Kwa mujibu wa Kanuni ya 9(1) ya Kanuni za Veterinari (Leseni ya Wakaguzi wa Nyama) ya Mwaka 2011; kutakuwa na ada ya kuhuisha itakayolipwa kila mwaka na mkaguzi wa nyama aliyeidhinishwa.

Daktari wa mifugo aliyesajiliwa, mtaalamu msaidizi aliyeorodheshwa na msaidizi wa mtaalam msaidizi aliyeandikishwa hawatalipa ada ya uhifadhi kulingana na Kanuni ya 9(2) ya Kanuni za Veterinari (Leseni ya Wakaguzi wa Nyama) ya Mwaka 2011.

Kuomba kuhuisha bofya hapa>>>>>http://mimis.mifugo.go.tz

 

Kuhuisha kwa Wataalam wa Maabara za Mifugo

Kwa mujibu wa Kanuni ya 5(1) ya Kanuni za Veterinari (Leseni ya Wataalamu wa Maabara ya Mifugo) ya Mwaka 2011, kutakuwa na ada ya kuhuisha itakayolipwa kila mwaka kwa Baraza na wataalamu wa maabara ya mifugo walio na leseni.

Ada ya kuhuisha inapaswa kulipwa katika mwaka wa kalenda;

Kiasi cha ada za kuhuisha kitalipwa kwa mujibu wa Kanuni ya Veterinari (Ada na Tozo Nyingine) ya Mwaka, 2015.

Kuomba kuhuisha bofya hapa>>>>>http://mimis.mifugo.go.tz

 

Kuhuisha kwa Vituo vya Huduma ya Mifugo

Kwa mujibu wa Kanuni ya 34 ya Kanuni za Veterinari (Usajili wa Madaktari wa Mifugo na Vituo vya Huduma za Mifugo) Kanuni za 2004; cheti cha usajili wa kituo cha afya ya wanyama kilichotolewa chini ya kanuni hizi kitakuwa halali mradi tu ada ya mwaka ya kuhuisha imelipwa.

Ada ya kuhuisha vituo vya huduma za mifugo inapaswa kulipwa katika mwaka wa fedha wa serikali.

Kiasi cha ada za uhifadhi na faini ya kuchelewa kuhuisha vitalipwa kulingana na Kanuni ya Veterinari (Ada na Tozo Nyingine) ya Mwaka, 2015.

Kuomba kuhuisha bofya hapa>>>>>http://mimis.mifugo.go.tz