MAFUNZO YA KUJIENDELEZA KITAALUMA (CPD)

Mafunzo ya Kujiendeleza Kitaaluma (CPD) ni shughuli yoyote ambayo hutoa thamani ya ziada kwa uwezo wa wataalamu kupitia kupata maarifa mapya, ujuzi na sifa za kibinafsi zinazohitajika kwa utekelezaji unaofaa wa majukumu ya kitaaluma na kiufundi.

Malengo ya CPD

Mafunzo ya Kujiendeleza Kitaaluma (CPD) yanalenga kuhakikisha:-

  1. Umahiri na ustadi katika majukumu ya taaluma
  2. Uzingatiaji wa kanuni na maadili za kitaaluma katika kutekeleza majukumu ya kitaaluma
  3. Upangaji wa kimkakati unaofaa kuzuia na kudhibiti magonjwa, afya shirikishi, afya ya jamii na usugu wa vimelea

Watoaji wa CPD

Katika kutoa mafunzo kwa ajili ya kuwaendeleza wataalamu wa afya ya wanyama, Baraza hushirikiana na Taasisi zenye ithibati zikiwemo:

  1. ALPHA ZOETIS, ambayo imeanzisha mafunzo ya muda mfupi kwa wataalamu kupitia tovuti ya www.zoetis.co.tz
  2. Chama cha Madaktari wa Mifugo Tanzania (TVA) na Chama cha Wataalamu Wasaidizi Tanzania (TAVEPA)
  3. Mtandao wa mafunzo ya kitaalam https://tva.wcea.education
  4. Chama cha Kulinda Wanyama Arusha (ASPA)
  5. Shirika la Wanyama Wadogo Tanzania (TASAVO)

Baraza bado linakaribisha washirika wengine ambao wako tayari kutoa kozi za CPD kwa ajili ya kuboresha taaluma ya mifugo. Kabla ya mafunzo ya CPD, Taasisi zinapaswa kuwasilisha maudhui ya mafunzo kwenye Baraza kwa ajili ya kuidhinishwa.

 

Wanaostahili Kufanya Mafunzo ya Kujiendeleza

 

Wataalamu wote wa mifugo ambao wamesajiliwa, kuorodheshwa au kuandikishwa na Baraza wanastahili kupata mafunzo ya CPD kila mwaka kulingana na Mwongozo wa Kufuatilia Mafunzo ya Kujiendeleza Kitaaluma kwa Madaktari wa Mifugo na Wataalamu Wasaidizi wa Mifugo, 2014.

Ili kupata mwongozo wa CPD bofya hapa>>Mwongozo