Huduma tunazotoa ni pamoja na:

(a) Kusajili Madaktari wa Mifugo, Madakatari wa Mifugo Wabobezi na vituo vya huduma ya afya ya mifugo;

(b) Kuandikisha Wataalamu wa Mifugo wasaidizi;

(c) Kuorodhesha Wasaidizi wa Wataalamu wa Mifugo Wasaidizi

(d) Kutoa leseni kwa wahimilishaji, wakaguzi wa nyama na wataalam wa maabara. 

(e) Kusimiamia huduma ya tiba ya wanyama na watoa huduma;

(f) Kutambua sifa za mafunzo, vituo vya mafunzo, taasisi za mafunzo na vyuo vya mafunzo ya mifugo;

(g) Kuainisha viwango vya chini vya vituo vya huduma za afya  ya mifugo;

(h) Kubainisha wigo wa shughuli za mazoezi ya Madaktari wa Mifugo, Wataalamu wa Mifugo, Wataalamu na Wasaidizi Wasaidizi;

(i) Kubainisha viwango vya chini vinavyohitajika kwa ajili ya mafunzo ya shahada, stashahada, astashahada au tuzo nyingine yoyote inayowapa haki wamiliki wake kutoa huduma za afya ya wanyama;

(j) Kuwa na udhibiti mzuri wa kinidhamu juu ya maadili ya kitaaluma na mwenendo wa huduma ya tiba ya wanyama;

(k) Kukuza na kuhimiza maendeleo ya elimu kuhusu utendaji wa Taaluma ya Veterinari;

(l) Kutoa taarifa na elimu kuhusu Taaluma ya Veterinari;

(m) Kuwezesha ushirikiano kati ya watu na mashirika yanayohusiana na taaluma ya veterinari ili kuimarisha hadhi na uadilifu wa taaluma ya veterinari;

(n) Kupanga na kuendesha mitihani ya ufaulu ili kujua umahiri katika elimu ya veterinari na vitendo;

(o) Kufuatilia utendaji kazi wa madaktari wa mifugo, wataalam wa mifugo wasaidizi, na Wasaidizi wa Wataalamu wa Mifugo Wasaidizi;

(p) Kumshauri na kutoa mapendekezo kwa Waziri mwenye dhamana ya mifugo kuhusu masuala yoyote yanayohusu tiba ya wanyama.

(q) Kushirikiana na taasisi au vyombo vingine vinavyohusika katika kutoa ithibati ya mtaala wa mafunzo, unaotoa sifa za usajili wa Madaktari wa Mifugo, uandikishaji wa Wataalamu  wa Mifugo asaidizi na uandikishaji wa Wasaidizi wa Wataalamu wa Mifugo Wasaidizi.