Kamati za Baraza zimeundwa chini ya Kifungu cha 6 (2) cha Sheria ya Veterinari SURA 319. Kila Kamati ina wajumbe sita (6) akiwemo Mwenyekiti na Katibu. Kamati za Baraza ni kama ifuatavyo:
(i) Kamati ya Usajili na Mitihani - hushughulikia masuala ya usajili, uandikishaji, uorodheshaji wa wataalamu na vituo vya huduma za afya ya mifugo na mitihani ya Baraza na vyuo.
(ii) Kamati ya Nidhamu - hushughulikia masuala ya nidhamu na maadili. ina jukumu la kufanya uchunguzi wa awali kama ilivyoainishwa chini ya Kifungu cha 45 cha Sheria. ya Veterinari
(iii) (iv) Kamati ya kusimamia Huduma na Vituo - inashughulikia huduma na vituo vya afya ya wanyama. Kushauri na kupendekeza kwa baraza juu ya viwango vya chini vya huduma ya afya ya mifugo kwa vituo vya afya ya wanyama na wigo wa shughuli za mhuduma na madaktari wa mifugo, wataalam wasaidizi wa mifugo na wasaidizi wa wataalamu wasaidizi.
(iv) Kamati ya Madawa na Chanjo - inahusika na dawa na chanjo. hushauri na kupendekeza kwa Baraza juu ya maswala yanayohusiana na dawa za mifugo, chanjo na vifaa.