24 Oct, 2023 Pakua

TAARIFA KWA UMMA

KUSUDIO LA KUFUTA MAJINA YA MADAKTARI WA MIFUGO NA WATAALAMU WA MIFUGO WASAIDIZI WASIOHUISHA USAJILI KWENYE REJESTA

Dodoma: 24 Oktoba, 2023

Baraza la Veterinari Tanzania chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi lilianzishwa kwa mujibu wa Kifungu cha 3 cha Sheria ya Veterinari (SURA 319).

Pamoja na majukumu mengine, Baraza la Veterinari Tanzania limepewa mamlaka ya kusajili, kusimamia, kufuatilia na kudhibiti Madaktari wa Mifugo na Wataalam wa Mifugo Wasaidizi. Kifungu 23(1) na 37(1) cha Sheria ya Veterinari (SURA 319) kinamtaka Daktari wa Mifugo na Mtaalam wa Mifugo Msaidizi aliyetambuliwa na Baraza kuhuisha Usajili kila mwaka kwa kulipia “Retention fees”.

Kifungo 23(4) na 37(3) kinaelekeza kuondolewa kwenye Rejesta Madaktari wa Mifugo na Wataalam wasaidizi wa Mifugo endapo hawatakuwa wamelipia ada ya kila mwaka.

Hivyo basi, Ofisi ya Msajili wa Baraza inawatangazia Madaktari wa Mifugo na Wataalam wa Mifugo Wasaidizi wote kuwa wanatakiwa kulipa ada ya mwaka kabla ya tarehe 15/11/2023. Watakaoshindwa kulipia Baraza linakusudia kuwafuta kwenye Rejesta.

Imetolewa na;

MSAJILI
BARAZA LA VETERINARI TANZANIA